Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Prof. Kabudi: Marekebisho Ya Viwanja Yakamilike Haraka

  • 49
Scroll Down To Discover

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi amewataka Wakandarasi wanaofanya marekebisho katika dimba la Benjamin Mkapa, Shule ya Sheria na uwanja wa Gymkhana waharakishe ili viwanja hivyo viwe tayari kwa ajili ya mashindano ya CHAN 2024 yatakayofanyika Tanzania, Kenya na Uganda Agosti mwaka huu .

Ameyasema hayo leo Mei 10, 2025 alipofanya ziara maalumu katika viwanja hivyo, akiongozana na Katibu Mkuu Wizara hiyo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa kwenye viwanja hivyo jijini Dar es salaam na akisema kuwa, uwanja wa Mkapa mpaka sasa ukarabati umefikia asilimia 85.

” Tumeanza na kiwanja shule ya Sheria vyumba vya kubadilishia nguo vimekamilika vimebaki mambo machache lakini ujenzi wa wavu wakuzuia mpira, changamoto kubwa tuliyokuwa nayo ilikuwa ni eneoa.kuchezea ( Pitch), viwanja hivi sio viwanja vya nyasi bandia au nyasi chotara ni vya nyasi asilia ambayo inahitaji utaalamu wa hali ya juu, kujua aina ya udongo ulionao aina ya maji yanayopatikana lakini pia kama unavyoona ni lazima kujua aina ya majani yanayopaswa kuwa pale. Amesema Prof. Kabudi.

Ameongeza kuwa, kazi ya ukarabati wa viwanja ambayo imefanywa na Kampuni ya Uturuki ya Reform Sports ambayo ina uzoefu mkubwa tu wa kujenga viwanja na wamefanya kazi hiyo katika nchi 160 na hapa Afrika, Tanzania ni nchi ya 16 na tayari wamefanya kazi Zanzibar na toka wameanza kwa kipindi cha mwezi wameonesha maendeleo makubwa na mpaka mwezi Mei viwanja vya mazoezi vya Shule ya Sheria na Gymkhana vitakuwa vimeshakamilika.

Aidha, Prof. Kabudi amesema mchezo wa fainali kati ya Simba dhidi ya RS Berkane utachezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa kwa sababu marekebisho yaliyoletwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika ( CAF) yamekamilika

Kuhusu kubadilisha viti kazi hiyo inaendelea vizuri tayari 38,000 vimebadilishwa na ndani ya muda mfupi eneo hilo litakuwa limejaa kwakua viti 20,000 vimeshaagizwa vipo njiani vinatarajia vifike tarehe 15 ya mwezi huu, baada ya hapo kazi ya kufunga itaendelea upande uliosalia na akiwahimiza wakandarasi tarehe 15 Juni 2025 kazi iwe imekamilika.



Prev Post MAGAZETI ya Leo Jumapili 11 May 2025
Next Post Charles Hillary, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Afariki Dunia
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook