
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth, amesema kuwa Marekani haina haraka kufikia makubaliano na Iran, huku akisisitiza msimamo mkali wa serikali yao kuhusu mgogoro unaoendelea.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Pentagon, Hegseth alisema Marekani haina presha ya kufanya makubaliano, akisisitiza kuwa muda hauwapi shinikizo na kwamba Iran ndiyo inapaswa kuchukua hatua.
Alieleza kuwa Iran inapaswa kukubali masharti yanayohusu kusitisha mpango wake wa nyuklia, akisema “mpira uko kwao” kufanya uamuzi huo.
Kauli hiyo inaashiria mabadiliko ya msimamo wa utawala wa Marekani, ambapo Rais Donald Trump pia amenukuliwa akisema hana shinikizo la haraka kufikia makubaliano ya kumaliza vita.
Mgogoro huo umeendelea kwa takribani miezi miwili bila dalili za Iran kuachana na mipango yake ya nyuklia, huku hali ya mvutano ikiendelea kuongezeka katika eneo la Mashariki ya Kati.
NETANYAHU AFANYIWA UPASUAJI WA TEZI DUME – AFICHUA MATIBABU YA SARATANI YA AWALI….
The post Pete Hegseth: Marekani Haina Haraka Kufikia Makubaliano na Iran appeared first on Global Publishers.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!