Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Video: Saba Wakamatwa kwa Tuhuma za Mauaji ya ‘Mungu Kuniyaa’ Mbarali

  • 7
Scroll Down To Discover


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa saba kwa tuhuma za kumuua Mungu Kuniyaa Mamboleo (38), mkazi wa Ihanga Mkanyageni, Wilaya ya Mbarali.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, tukio hilo lilitokea Aprili 21, 2026 majira ya saa 3:00 usiku katika Mtaa wa Ihanga Mkanyageni, Kata na Tarafa ya Rujewa, baada ya kundi la watu linalodaiwa kuongozwa na Samweli Yohana maarufu “Fagu” (22) kuvamia kambi ya kufugia ng’ombe na kumshambulia marehemu kwa silaha za jadi hadi kusababisha kifo chake.

Polisi ilianzisha msako mara baada ya tukio hilo na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa saba akiwemo Samweli Yohana pamoja na Advero Seng’unda (40), Shija Gidingi (25), Patrick Yonga (44), Gasper Mashaka (29), Neno Paulo (35) na Msifuni Ezekia (32), wote wakazi wa Ihanga Mkanyageni.

Uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha tukio hilo ni tuhuma za wizi wa ng’ombe, huku wananchi wakidaiwa kujichukulia sheria mkononi. Polisi imeeleza kuwa upelelezi unaendelea ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa.

Katika tukio lingine, Mahakama ya Wilaya ya Kyela imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Brown Frank Mwaitubi (31), mkazi wa Kajunjumele, baada ya kupatikana na hatia ya kuwa na dawa za kulevya aina ya bangi kete 20 zenye uzito wa gramu 896.35.

Hukumu hiyo ilitolewa Aprili 24, 2026 na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mhe. Rosta Emmanuel Mofuga. Ilielezwa mahakamani kuwa mshtakiwa alikamatwa Agosti 18, 2025 akiwa amehifadhi bangi nyumbani kwake kwa lengo la kuuza.

Mahakama ilimtia hatiani kwa mujibu wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Dawa za Kulevya, Sura ya 95 (marejeo ya mwaka 2023).

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limetoa wito kwa wananchi kutojichukulia sheria mkononi, badala yake kuwafikisha watuhumiwa katika vyombo vya sheria, na pia kujiepusha na biashara na matumizi ya dawa za kulevya kutokana na athari zake na adhabu kali zinazotolewa kisheria.

The post Video: Saba Wakamatwa kwa Tuhuma za Mauaji ya ‘Mungu Kuniyaa’ Mbarali appeared first on Global Publishers.



Prev Post Matangazo ya Dira ya Dunia Redio
Next Post Pete Hegseth: Marekani Haina Haraka Kufikia Makubaliano na Iran
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook