Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Familia Yalia: Sindano 15 Kila Siku, Msichana Ahitaji Msaada, Ateseka Miaka 18 – Video

  • 7
Scroll Down To Discover

Msichana Mariam Magomi, mkazi wa Sinza C jijini Dar es Salaam.

Msichana Mariam Magomi, mkazi wa Sinza C jijini Dar es Salaam, anaishi katika maumivu makali kwa zaidi ya miaka 18 kutokana na tatizo linalomzuia kupata haja kubwa kama watu wengine.

Kwa kipindi hicho chote, Mariam amefanyiwa upasuaji zaidi ya mara 20 kwenye tumbo lake, lakini bado hali yake inaendelea kuwa ngumu na inahitaji matibabu ya kina zaidi. Ili kuweza kuhimili maumivu, analazimika kutumia sindano zaidi ya 15 kila siku.

Kwa sasa, anahitaji kusafirishwa kwenda India kwa matibabu maalum. Familia yake imetumia fedha nyingi na hata kuuza mali zao ili kujaribu kuokoa maisha yake, huku gharama za matibabu na dawa zikiwa kubwa na zinaendelea kuongezeka.

Hali hii imegusa wengi kutokana na changamoto anazopitia kila siku, na bado anahitaji msaada wa kifedha ili kuweza kupata matibabu yanayoweza kumrudisha katika maisha ya kawaida.

📞 Kwa yeyote atakayeguswa na hali yake, unaweza kuchangia kupitia namba zifuatazo:

  • 0764 769742 (Brigita Magomi)
  • 0685 379888 (Brigita Magomi)

The post Familia Yalia: Sindano 15 Kila Siku, Msichana Ahitaji Msaada, Ateseka Miaka 18 – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post Pete Hegseth: Marekani Haina Haraka Kufikia Makubaliano na Iran
Next Post Waziri wa Iran Aelekea Pakistan, Russia na Oman Kukuza Ushirikiano wa Kikanda
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook