Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Video: Mbunge Bahati Ndingo Aibananisha Serikali Sekta ya Elimu

  • 11
Scroll Down To Discover

Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Bahati Ndingo akimuuliza swali Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba, Bungeni Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Bahati Ndingo, amepata nafasi ya kumuuliza swali Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwigulu Nchemba, kuhusu sekta ya elimu.

Katika swali lake, Mbunge huyo alieleza kuwa mtaala mpya wa elimu unatarajiwa kusababisha ongezeko kubwa la wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza mwaka wa masomo 2027, kutokana na wanafunzi wa darasa la sita na la saba kujiunga kwa pamoja kwa mara ya kwanza tangu maboresho ya mtaala wa elimu ya msingi.

Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu Mwigulu alimpongeza Mbunge huyo kwa ufuatiliaji mzuri wa masuala ya wananchi, na kuahidi kuwa Serikali imejipanga kukabiliana na changamoto ya ongezeko hilo la wanafunzi.

Alisema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kujenga miundombinu ya shule pamoja na kuajiri walimu kwa wingi ili kuhakikisha wanafunzi wote wanapata nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari.

The post Video: Mbunge Bahati Ndingo Aibananisha Serikali Sekta ya Elimu appeared first on Global Publishers.



Prev Post SBL Yatambulisha Serengeti Premium Apple Kwa Wadau Dar
Next Post NASA Yaandika Historia Tena, Yazindua Misheni ya Artemis II Kuelekea Mwezini
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook