Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia Atangaza Fursa za Uwekezaji Tanzania Mbele ya Viongozi wa Dunia

  • 18
Scroll Down To Discover

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa hakikisho la miundombinu bora ya uwekezaji nchini kwa wawekezaji duniani, akisema Tanzania imewekeza vema katika ujenzi wa reli, nishati, bandari na miundombinu ya uchukuzi.

 

Miundombinu mingine aliyosema imewekezwa nchini ni kutengwa kwa maeneo maalumu ya uwekezaji na dirisha moja la uwekezaji, yote hayo yamefanywa ili kujenga mazingira rafiki kwa wawekezaji wa muda mrefu.

Dkt Samia ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo, Jumatano Februari 4, 2026 alipozungumza katika uzinduzi wa Jukwaa la Uwekezaji Duniani kwa upande wa Afrika (GAIS), linalofanyika Dubai, katika Taifa la Falme za Kiarabu.

 

Amesisitiza wawekezaji hawatafuti fursa pekee, bali uaminifu uthabiti wa sera, taasisi imara na Serikali zinazotekeleza ahadi zake, akidokeza Tanzania ina sifa zote hizo.

 

Ushiriki wa Tanzania katika GAIS unaakisi dhamira ya nchi ya kwenda kwenye ushirikiano uliopangiliwa vema na unaoendana na vipaumbele vya maendeleo ya taifa na matarajio ya wawekezaji wa kimataifa.

 

The post Rais Samia Atangaza Fursa za Uwekezaji Tanzania Mbele ya Viongozi wa Dunia appeared first on Global Publishers.



Prev Post Rais Samia Akizungumza Jambo na Makamu Rais wa UAE
Next Post Makamu Nchimbi Kwenye Mazishi ya Munde Tambwe Tabora
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook