KOCHA Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amesema anaridhishwa kwa kiwango kikubwa na kiwango cha uchezaji wa kikosi chake licha ya matokeo ya sare dhidi ya Esperance de Tunis katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Barker amesema wachezaji wake walionyesha moyo mkubwa wa ushindani, nidhamu ya hali ya juu pamoja na ujasiri mkubwa dhidi ya mpinzani mwenye uzoefu mkubwa katika mashindano ya kimataifa.
Barker ameeleza kuwa Simba ilianza mchezo kwa kasi, huku mipango waliyojiandaa nayo ikifanya kazi kwa sehemu kubwa ya dakika za mchezo. timu yake iliweza kushambulia kwa ufanisi na wakati huohuo kuwadhibiti Esperance, jambo lililowafanya washindwe kucheza kwa uhuru wao wa kawaida.
“Presha tuliyoitengeneza iliwalazimu wapinzani kufanya makosa na kushindwa kucheza kwa mtiririko wao wa kawaida. Mabao tuliyoruhusu yalitokana na mapungufu madogo ya kiulinzi ambayo yaliigharimu timu,” amesema Barker.
Kocha huyo alisisitiza kuwa makosa hayo ni ya kawaida katika michezo ya ushindani wa kiwango cha juu na akaweka wazi kuwa benchi la ufundi litayafanyia kazi haraka kabla ya michezo inayofuata.
Aliwapongeza mashabiki wa Simba kwa mchango wao mkubwa, akisema mazingira ya Uwanja wa Benjamin Mkapa yaliwapa nguvu wachezaji wake na kuwafanya wapambane kwa dakika zote 90 bila kukata tamaa.
Kwa upande wa mwelekeo wa mashindano, Barker amesema bado hakuna kitu kimeisha, kwani nafasi ya Simba kusonga mbele bado ipo wazi. kuwa timu itaendelea kupambana katika mechi zijazo kwa lengo la kupata matokeo bora na kutimiza malengo ya msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Tutafanya kazi kwa bidii, kurekebisha makosa na kuhakikisha Simba inaendelea kuwa timu shindani barani Afrika. Kwa umoja wa wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki, ninaamini Simba inaweza kufika mbali zaidi hapo baadae,” amesema Barker
The post BARKER ARIDHISHWA NA KIWANGO appeared first on Soka La Bongo.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!