NAHODHA wa Yanga SC, Dickson Job, amesema kuwa pointi moja waliyoipata dhidi ya Al Ahly inaweza kuwa muhimu katika mipango yao ya kufuzu hatua ya robo fainali, lakini hakuna anayepaswa kudhani mchezo umeisha.
Yanga walilazimishwa sare ya bao 1-1 nyumbani dhidi ya Al Ahly katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, mchezo uliojaa ushindani mkubwa na shinikizo la kila upande.
Job amesema kuwa licha ya matokeo hayo, kikosi chake kina mechi mbili muhimu mkononi na kina imani ya kufanikisha malengo yake.
“Kikubwa ni kushikamana na nafasi tuliyo nayo ya kwenda kucheza robo fainali. Tuna michezo miwili mbele, tuwe wamoja, tunaenda kupambana kupata pointi sita hizo,” amesema Job.
Mchezo ujao wa Yanga utakuwa ugenini dhidi ya AS Far Rabat, timu inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 5. Mshindi wa mchezo huo atafungua ukurasa wa moja kwa moja wa kufuzu hatua ya robo fainali, jambo linaloweka shinikizo kubwa lakini pia fursa ya kipekee kwa Yanga.
Job ameongeza kuwa: “Hii sare ya Al Ahly si mwisho, bali ni mwanzo wa kampeni. Tunapaswa kuonyesha umoja, nidhamu na ubora wa kiufundi ili kufanikisha ndoto ya robo fainali.”
Yanga sasa inaangalia mbele, ikiwa na azma ya kuonyesha nguvu ya kikundi na kuhakikisha ndoto ya robo fainali inakuwa kweli msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Timu hiyo itakabiliana na AS Far Rabat ugenini Februari 7 na kumalizia na JS Kabylie uwanja wa New Amaan Complex Februari 13
The post JOB, POINTI YA AL AHLY INAWEZA, NJIA ROBO FAINALI appeared first on Soka La Bongo.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!