Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Watendaji Kituo Cha Uokozi Mwanza Watakiwa Kutoa Huduma Za Dharura Kwa Saa 24

  • 24
Scroll Down To Discover

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa maagizo kwa watendaji wa Kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokozi cha Kikanda – Mwanza, chenye thamani ya takribani shilingi bilioni 19.8, kuhakikisha kituo hicho kinaendeshwa kwa saa 24 na kwa ufanisi wa hali ya juu.

Amesema hayo leo Januari 23, 2026 baada ya kutembelea kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokozi, jijini Mwanza

Amesisitiza kuwa huduma za uokozi ni kazi ya kuokoa maisha, hivyo hakuna uvumilivu kwa uzembe, kuchelewesha utoaji wa huduma za msaada pindi inapohitajika.

“Hii ni kazi ya kuokoa maisha. Uzembe, kusinzia au kuchelewesha kutoa msaada ni kuhatarisha maisha ya Watanzania. Kituo hiki lazima kifanye kazi saa 24.”

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema ujenzi wa kituo hicho ni uthubitisho wa dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwatumikia watanzania na kujali changamoto mbalimbali nchini.

“Kituo hiki kilikuwa kijengwe mwaka 2018 kwenda Mwaka 2020, kilisimama baada ya wenzetu kujitoa, lakini Rais Dkt. Samia akasema tutakijenga kituo hiki kwa fedha zetu ili wavuvi waweze kupata huduma ya usalama katika kazi zao”.

The post Watendaji Kituo Cha Uokozi Mwanza Watakiwa Kutoa Huduma Za Dharura Kwa Saa 24 appeared first on Global Publishers.



Prev Post Marekani yajiondoa rasmi W.H.O. Katika Dira ya Dunia
Next Post BBC yathibitisha mauaji ya waandamanaji Iran. Katika Dira ya Dunia TV
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook