Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

SILAHA MPYA YANGA KUITUIKIA FAINALI YANGA MAPINDUZI

  • 33
Scroll Down To Discover

UONGOZI wa klabu ya Yanga umeeleza kuwa upo tayari kuwatumia wachezaji wake wapya waliosajiliwa hivi karibuni katika michezo ya hatua za juu ya Kombe la Mapinduzi linaloendelea visiwani Zanzibar.

Yanga tayari imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika michezo ya awali, hali inayowaweka katika nafasi nzuri ya kupigania taji hilo.

Katika hatua ya nusu fainali, Yanga inatarajiwa kuivaa Singida Black Stars Januari 9, 2025, kwenye uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe, amesema mashabiki wa Yanga wanapaswa kutarajia kuona mabadiliko ndani ya kikosi, ikiwemo uwezekano wa kuonekana kwa wachezaji wapya kuanzia nusu fainali hadi fainali.

Kamwe amesema  uwepo wa wachezaji wote kambini, wakiwemo waliosajiliwa hivi karibuni, umeipa benchi la ufundi uhakika mkubwa wa kupanga kikosi chenye ushindani.

“Hii ni hatua muhimu kwetu na tunakwenda kukutana na wapinzani wenye uwezo, lakini wachezaji wote wapo tayari, hata wale wapya, hivyo yeyote tutakayekutana naye atapata wakati mgumu,” amesema  Kamwe.

Yanga inaingia kwenye hatua hizi za maamuzi ikiwa na dhamira ya kutwaa Kombe la Mapinduzi, huku wachezaji wapya wakitajwa kuwa silaha muhimu katika kufanikisha azma hiyo.

The post SILAHA MPYA YANGA KUITUIKIA FAINALI YANGA MAPINDUZI appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post KISASI CHA KIVITA NA HESHIMA AZAM NA SIMBA
Next Post ECUA AIBEBA YANGA NUSU FAINALI
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook