Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Video Vixen Genno Acharuka “Nilikopwa Kwenye Video ya Diamond na Baba Levo” – Video

  • 64
Scroll Down To Discover

Video vixen maarufu Genno ameibua gumzo baada ya kufichua kuwa aliwahi kukopwa malipo katika moja ya video aliyocheza akiwashirikisha wasanii wakubwa, akiwemo Diamond Platnumz na Baba Levo.

Genno amesema alipata nafasi hiyo kupitia mwandaaji wa video ambaye hakutaka kumtaja jina, lakini licha ya kufanya kazi kwa weledi, hakuwahi kulipwa kama walivyokubaliana.

Vixen huyo ambaye amekuwa akitokea kwenye video nyingi za wasanii wakubwa kama Harmonize, Balaa MC na wengine, amefunguka mambo mengi kuhusu safari yake ya kazi, changamoto anazokutana nazo, pamoja na namna tasnia ya video vixens ilivyo na changamoto nyingi zisizoonekana hadharani.

Katika mahojiano hayo, Genno pia ametumia nafasi hiyo kuwashauri vijana kuzingatia kazi zao na kutumia muda wao kujijenga badala ya kujiingiza kwenye mambo yasiyo na tija.

“Vijana muda ni mali, tumieni vipaji vyenu kujenga maisha yenu. Tusipoteze nguvu kwenye vitu ambavyo havitusaidii,” amesema.

Kauli yake imepokelewa kwa hisia tofauti, huku mashabiki wengi wakimsifia kwa ujasiri na uwazi.

The post Video Vixen Genno Acharuka “Nilikopwa Kwenye Video ya Diamond na Baba Levo” – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Akagua Uharibifu Kwenye Kituo cha Polisi Kikatiti Arusha
Next Post Dkt. Mwigulu Awasili KIA Kukagua Madhara ya Vurugu za Arusha
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook