
Katika ukumbi wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jana taifa lilishuhudia tukio lenye thamani ya kipekee katika historia ya uongozi wa kisasa. Mbele ya Bunge Tukufu, Mhe. Eric James Shigongo aliapa kwa moyo wa uzalendo, uaminifu, na dhamira thabiti ya kulitumikia Taifa la Tanzania.
Kitabu cha Katiba mkononi na moyo uliojaa heshima kwa wananchi waliomwamini vilikuwa ishara tosha ya ujasiri, uwajibikaji na nia njema ya kulinda maslahi ya Watanzania wote. Sauti yake iliposikika akila kiapo, haikuwa sauti ya mtu mmoja, bali sauti ya maelfu ya wananchi wa Buchosa waliompa dhamana ya kuwawakilisha sauti ya matumaini, maendeleo na mabadiliko chanya.
Mhe. Shigongo wakati akiwa katika kampeni zake aliahidi kuendeleza siasa za maendeleo zenye kuunganisha watu, huku akisisitiza umuhimu wa amani kama msingi wa mafanikio ya kizazi cha sasa na kijacho. Ni matumaini ya wengi kwamba uongozi wake utaendelea kuwa chachu ya mabadiliko na dira ya maendeleo ya kweli kwa wana Buchosa.












Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!