

Wabunge wa Bunge la Kumi na Tatu walivyowasili katika viwanja vya Bunge, Jijini Dodoma, leo Novemba 12, 2025, kwa ajili ya Kikao cha Pili cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge hilo jipya.
Kikao hiki kinatarajiwa kuendelea na shughuli za awali za Bunge ikiwemo kuapishwa kwa wabunge waliobaki, kuundwa kwa kamati mbalimbali za kudumu, na masuala mengine ya utaratibu wa kuanza rasmi kwa shughuli za Bunge la 13 baada ya kufunguliwa rasmi wiki iliyopita.
Tukio hili limevutia hisia za wengi kutokana na muundo mpya wa Bunge baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, ambapo wabunge wapya na wale waliorejea wanatarajiwa kuanza majukumu yao kwa pamoja.












Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!