

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amesema hakuna makubaliano yoyote yaliyofanyika kati yao na Jeshi la Polisi kuhusu kuachiwa kwao kwa dhamana hapo jana.
Akizungumza leo (Novemba 11, 2025) nje ya Kituo Kikuu cha Polisi (Central) jijini Dar es Salaam, Heche amesema wamefika kituoni kama walivyoelekezwa wakati wa kuachiwa kwao jana.
“Kama tulivyokamatwa ndivyo tulivyoachiwa. Hakuna mazungumzo yoyote tuliyofanya na mtu yeyote,” alisema Mhe. Heche.
Viongozi hao wa CHADEMA, akiwemo Heche, walikamatwa mwishoni mwa wiki wakiwa pamoja na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho kabla ya kuachiwa kwa dhamana jana jioni.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!