

Mbunge wa Jimbo la Ilala, (CCM) Mhe. Mussa Azzan Zungu, amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata kura 378 kati ya kura 383 zilizopigwa.
Uchaguzi huo umefanyika leo, Novemba 11, 2025, katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma, ambapo Zungu amewashinda wagombea wengine watano waliokuwa wakipeperusha bendera za vyama vya NRA, DP, ADC, NLD, na AAFP.
Zungu atakuwa kiongozi wa Mhimili huo katika Bunge la 13 ambalo limeanza rasmi leo.
Ikumbukwe kuwa, Zungu amekuwa Naibu Spika wa Bunge hilo kuanzia mwaka 2022 na sasa anarithi mikoba ya aliyekuwa Spika wake, Dkt. Tulia Ackson ambaye alijiondoa kwenye kinyang’anyiro












Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!