Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hamza Johari Aapishwa Kuwa Mbunge

  • 14
Scroll Down To Discover

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amekula kiapo cha Uaminifu mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Musa A. Zungu, tarehe 11 Novemba, 2025. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameapishwa kuwa Mbunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa kumi na tatu(13) wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameapishwa kwa mujibu wa Ibara ya 59(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 inayompa Mamlaka ya kuwa Mbunge na kuhudhuria vikao vya Bunge.

Aidha, Uapisho huo mbele ya Bunge wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, unafuatia Uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kumteua Mhe. Hamza S. Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali mnamo tarehe 3 Novemba, 2025 na kufuatiwa na uapisho uliofanyika tarehe 5 Novemba, 2025 Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma.



Prev Post Familia Ya Rais Aliyepinduliwa Yasomewa Kesi Ya Ufisadi
Next Post Heche azungumzia kwa mara ya kwanza kuachiwa kwao na Jeshi la Polisi – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook