Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Waziri Mkuu Majaliwa Akagua Huduma za Mabasi ya Mwendokasi Kivukoni – Video

  • 3
Scroll Down To Discover

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mabasi mapya 60 ya Mwendokasi kutoka kampuni ya Mofat yataongezwa katika barabara ya Kivukoni-Kimara na kufikisha jumla ya mabasi 90 yatakasafirisha abiria katika barabara hiyo.

Majaliwa ameyasema hayo leo Oktoba 02, 2025 alipofika kukagua na kujionea hali ya usafiri na usafirishaji katika kituo cha Kivukoni na Kimara Mwisho.

“tumeona upungufu mkubwa wa kutoka Kivukoni mpaka Kimara tulikuwa tuna mabasi 32 mpaka jana yamebaki mabasi 30 ni kweli hayatoshi lakini tumeona tuchukue mabasi 60(ya kampuni ya Mofat) yaingie kwenye barabara hii tutakuwa na jumla ya mabasi 90 tunaamini ugumu huu utapungua kwa kiasi kikubwa” amesema Majaliwa

Majaliwa ameongeza kuwa malengo ya serikali ni kupunguza na ikiwezekana kuondoa kabisa changamoto hiyo. “malengo yetu ni kuondoa kadhia hii”

Ameeleza kuwa kampuni ya UDART ambayo ndiyo ilikuwa inasafirisha abiria kwa barabara hiyo tayari imeagiza magari mengine na muda wowote yataingia nchini. Huku akisisitiza usimamizi madhubuti wa miundombinu na huduma hizo.

Pamoja na hayo ametaka kuhakikishwa ukamilishwaji na uthabiti wa uwekwaji wa miundombinu ya kielektroniki katika vituo vya kukatia tiketi ili kuepuka matumizi ya fedha taslim(cash) bali zitumike kadi.

“njia ya utozaji nauli itakuwa electronic badala ya fedha cash(taslim) kuziba mianya ya kupokea fedha kwa njia ya mkono” amesema Majaliwa.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Mofat Muhammad Abdallah Kassim ameeleza kuwa kufikia asubuhi ya leo tayari wameingiza magari 20 barabarani na kufikia leo jioni watakuwa wamekamilisha magari 60.

 



Prev Post Rais Samia Avunja Bodi Ya DART na UDART, Ateua Wenyeviti Wapya
Next Post Dkt. Nchimbi Ndani ya Jimbo la Nanyamba, Mtwara
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook