Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

DILI LA MUKWALA KUUZWA…SIMBA WANAPIGA PESA NDEFUU AISEE….MBADALA WAKE HUYU HAPA…

  • 7
Scroll Down To Discover

DIRISHA la usajili la usajili linatarajiwa kufungwa usiku wa leo, huku kukiwa na sapraizi kubwa kwa klabu ya Simba baada kutema mastraika wawili walioibeba timu hiyo msimu uliopita, huku winga aliyekuwa akitajwa huenda angefyekwa, akisalimika kama zali.

Ipo hivi. Msimu uliopita, Simba iliongozwa eneo la mbele ya washambuliaji Steven Mukwala na Leonel Ateba kila mmoja akifunga mabao 13 sawa na aliyomaliza nayo Jonathas Sowah aliyekuwa Singida Black Stars kabla ya kutua Msimbazi kwa ajili ya kikosi cha msimu ujao.

Nyota hao wawili kila mmoja pia aliasisti mara nne, lakini timu ikiwa kambini Misri, Ateba aliaga baada ya kupigwa bei Al Shorta ya Iraq kisha akashushwa Seleman Mwalimu ‘Gomes’ kwa mkopo akitokea Wydad Casablanca ya Morocco.

Hivi unavyosema taarifa hii ni kwamba mabosi wa klabu hiyo wamempiga bei Mukwala kwa klabu ya Al Ittahad ya Libya na muda wowote taarifa itatolewa rasmi, lakini winga aliyekuwa akielezwa alikuwa atolewe Joshua Mutale akisalimika.

Simba ilishapitiliza idadi ya wachezaji 12 wa kigeni kama inavyotakiwa kwa kanuni za usajili wa Ligi Taarifa ni kwamba kabla ya dirisha la usajili kufungwa usiku wa leo, ni kwamba Mukwala amepigwa bei Al Ittihad ya Libya na ilikuwa inasubiriwa tu kutangazwa rasmi.

Mukala aliyeasisti pia mabao manne kama ilivyokuwa kwa Ateba, msimu uliopita licha ya kutumika kwa dakika chache, taarifa zilidokeza kuwa hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba msimu ujao 2025/26.

Inaelezwa kwamba Simba ilipokea ofa ndefu kutoa Al Ittihad ya Libya ambayo imetuma ofa ya kumnasa mshambuliaji huyo na kuwa sehemu ya kikosi chao msimu huu.

Chanzo cha kuaminika kutoka Simba kimesema kuwa Al Ittihad wamefika dau la kumnunua mshambuliaji huyo na dili hilo linatajwa kukamilikajana na uthibitisho utatolewa.

“Ni kweli tumefikia makubaliano ya kumuuza Mukwala kwenda Al Ittihad na kuna uwezekano akasajiliwa mchezaji mmoja ambaye atapishana na Mukwala kama kocha alivyosisitiza kuongezwa mchezaji mmoja,”kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Tumemuuza Mukwala kwa dau nono sana siwezi kuweka wazi ni kiasi gani lakini pesa hiyo itatusaidia kunasa saini ya mchezaji mwingine yeyote bora kama ambavyo kocha Fadlu amesisitiza kusajiliwa mchezaji mwenye ubora mkubwa.”

Mukwala ambaye wakati anatua Simba iliripotiwa amesaini mkataba wa miaka mitatu, tayari ametumikia mwaka mmoja na kuisaidia timu hiyo kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kupoteza mbele ya RS Berkane ya Morocco.

“Makubaliano ya pande zote mbili kati yetu sisi Simba na Al Ittihad yanakwenda vizuri nafikiri taarifa ya usahihi zaidi kama dili limekwenda kama lilivyopangwa kesho (leo) itatolewa na kila mwanasimba ataupongeza uongozi kwa biashara nzuri tuliyoifanya.”

Hata hivyo taarifa kutoka vyanzo vingine vinadai kuwa Simba watavuna karibu dola za kimarekni milioni moja sawa au zaidi ya Bilioni 2.5 za kitanzania kwa kumuuza nyota huyo anayechezea pia timu ya Taifa ya Uganda.

Taarifa zinasema kuwa Simba wameongeza maongezi juu ya kumpata nyota mwingine wa Uganda, John Okello anayechezea klabu ya Vipers ili kuwahi dirisha la usajili kabla halijafungwa leo saa sita usiku.

Hivi karibuni kocha, Fadlu alikaririwa akisema kuwa bado wanahitaji angalau mchezaji mmoja mwenye kitu cha ziada (X-Factor) atakayewaongezea kitu hasa kwenye michuano ya kimataifa pamoja na mbio za ubingwa wa ligi.

Hivyo kuuzwa kwa Mukwala kunatoa nafasi kwa Simba kufanya usajili mapema kabla ya dirisha la usajili la ndani halijafungwa.

Credit:- MwanaSpoti.

The post DILI LA MUKWALA KUUZWA…SIMBA WANAPIGA PESA NDEFUU AISEE….MBADALA WAKE HUYU HAPA… appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post YANGA WAIPIGA SIMBA BAO ‘ISHU’ YA UWANJA….ISHU NZIMA IKO HIVI….
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 08 , 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook