Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Brela Na Tmda Kushirikiana Katika Nyanja Ya Miliki Bunifu

  • 9
Scroll Down To Discover

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), wametia saini makubaliano ya ushirikiano katika nyanja ya miliki bunifu, kwa lengo la kuhakikisha wamiliki wa bidhaa wanalindwa kupitia usajili wa alama za biashara sambamba na vibali vya matumizi ya dawa na vifaa tiba.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo, tarehe 12 Agosti 2025 na Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa na Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dkt. Adam Fimbo, mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Bw. Nyaisa ameeleza kuwa, ushirikiano huo unalenga kuongeza ufanisi na tija kwa taasisi hizo kupitia kubadilishana taarifa za alama za biashara zilizosajiliwa na zinazotumika kwenye dawa na vifaa tiba, kufanya kaguzi elimishi za pamoja, kutoa mafunzo, kubadilishana uzoefu na kuhamasisha umma kuhusu haki za miliki bunifu.

Amefafanua kuwa, BRELA inapotoa usajili wa alama, mmiliki hupata haki ya kipekee na kuzuia wengine kuitumia. Hali hiyo, inapohusisha majina ya dawa inaweza kusababisha majina ya dawa yasiyoruhusiwa kumilikiwa binafsi kusajiliwa kama alama za biashara, jambo linaloweza kuwanyima wadau wengine haki ya kutumia majina hayo kwenye bidhaa zao.

“Katika mazingira ya sasa ya maendeleo ya viwanda, biashara na teknolojia, taasisi haziwezi kufanikisha majukumu yake kwa kujitenga. Ushirikiano huu utaboresha utoaji huduma, ulinzi wa haki za wabunifu wa alama zinazotumika katika dawa na vifaa tiba, na kuchochea ubunifu wa kiteknolojia na kibiashara nchini,” amesema Bw. Nyaisa.

Kwa upande wake, Dkt. Fimbo ameeleza kuwa ingawa BRELA na TMDA zimeanzishwa kwa sheria tofauti, baadhi ya majukumu yao yanashabihiana, hususan katika kulinda alama za biashara na hataza. Kupitia mashirikiano hayo, itakuwa rahisi kutambua bidhaa sokoni na kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini.

“Tumeanzisha mashirikiano haya kwa kuwa BRELA inasimamia usajili wa alama za biashara na utoaji wa hataza, huku TMDA ikihakikisha bidhaa za dawa zinakuwa na usajili wa hataza na alama husika. Hii itarahisisha utambuzi na ulinzi wa bidhaa zinazozalishwa na wazalishaji wa ndani na kudhibiti usambazaji wa bidhaa zisizotambulika nchini,” amesema Dkt. Fimbo.



Prev Post Harambee ya CCM Yafikia Bilioni 86, Malengo Bilioni 100 Kabla ya Uchaguzi – Video
Next Post CHADEMA Arusha Yawafukuza Wanachama 12 kwa Ukiukaji wa Katiba na Maadili
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook