Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

CHADEMA Arusha Yawafukuza Wanachama 12 kwa Ukiukaji wa Katiba na Maadili

  • 9
Scroll Down To Discover

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Arusha Mjini kimechukua hatua kali za kinidhamu dhidi ya jumla ya wanachama kumi na wawili (12), wakiwemo watano waliokuwa bado hawajajiondoa kwenye chama na saba waliokimbia chama kwa kujiunga na vyama vingine wakati mashauri yao ya kinidhamu yakiwa yanaendelea.

Kwa mujibu wa taarifa ya Agosti 12, 2025 iliyosainiwa na Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Arusha Mjini, Francis Chuma, kikao cha kawaida cha Kamati ya Tendaji kilichofanyika tarehe 2 Agosti 2025 na kilichosimamiwa na Mwenyekiti wa Wilaya, kilijadili mashauri ya kinidhamu na kuazimia kuwafukuza wanachama waliokiuka Katiba, Itikadi na Maadili ya chama.

Taarifa hiyo imeelezwa kuwa waliofutwa uanachama ni watano ni Amina Abubakar, Linus Antony, Boniphas Kimario, Hamisi Kidoleso na Emmanuel Assey, aliokimbia mashauri ya kinidhamu ni wawili ambao ni Martha Masoi na Emma Kimambo. Waliojiondoa na kujiunga na vyama vingine ni watano ambao ni Amani Kimath, Shaban Mipilo, John Lema, Jacklini Kimambo (wote wamejiunga na CHAUMMA) na Yasini Selemani (amejiunga na CCM).

CHADEMA imesisitiza kuwa ingawa uanachama wa chama cha siasa ni wa hiari, haikubaliki mwanachama kubaki ndani ya chama huku akijihusisha na shughuli za chama kingine, jambo linaloitwa ‘double agent’.

Taarifa hiyo imekumbusha kuwa yeyote atakayekwenda kinyume, aidha kwa kushirikiana na waliotajwa au kushiriki vitendo vya usaliti, atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za CHADEMA.



Prev Post Brela Na Tmda Kushirikiana Katika Nyanja Ya Miliki Bunifu
Next Post Wasanii na Wadau wa Urembo Wajitosa Kuchangia Milioni 20 katika CCM Gala Dinner 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook