Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

#Live: Shauri La Jinai Jamhuri Vs Tundu Lissu, Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu…

  • 5
Scroll Down To Discover

 

Dar es Salaam – Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, inaendelea leo Jumatano, Agosti 13, 2025, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo Hakimu Mfawidhi Franco Kiswaga anatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili.

Uamuzi huo unakuja baada ya upande wa utetezi kupinga ombi la upande wa mashtaka la kuahirisha mara kwa mara shauri hilo bila kupeleka suala hilo Mahakama Kuu iwapo bado wanakusudia kuendelea nalo.

Ikumbukwe kuwa Agosti 4, 2025, Mahakama Kuu – Masijala ya Dar es Salaam, ilikubali ombi la Jamhuri la kuficha majina na taarifa nyingine za mashahidi wa upande wa mashtaka, hatua iliyozua mjadala mpana kuhusu uwazi wa mashauri ya jinai yanayohusu viongozi wa kisiasa.

Kesi hii inasubiriwa kwa hamasa kubwa na wafuasi wa CHADEMA, wadau wa siasa na wanaharakati wa haki za binadamu, ikizingatiwa kuwa matokeo yake yanaweza kuwa na athari za moja kwa moja kwenye mustakabali wa kisiasa wa Lissu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 13, 2025
Next Post Harambee ya CCM Yafikia Bilioni 86, Malengo Bilioni 100 Kabla ya Uchaguzi – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook