Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Samia aahidi kuifanya Kigoma kuwa kitovu cha biashara

  • 4
Scroll Down To Discover

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kuifanya Mkoa wa Kigoma kuwa Kitovu cha biashara Ukanda wa Ziwa Tanganyika.

Akizungumza kwenye kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, amesema Serikali inafanya mambo mengi kuhakikisha kuuinuia mkoa huo, ikiwemo kufanya ukarabati wa reli za zamani, pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR.

“Ahadi yetu kwa Kalinzi na Kigoma kwa ujumla, mkitupa ridhaa kuongoza serikali lengo letu ni kuifanya Kigoma kuwa kitovu cha biashara kwenye Ukanda huu na ndio maana tunafanya ukarabati wa reli ya zamani, tunaleta reli ya kasi na tunaiunganisha na nchi jirani ili Kigoma ifanye biashara na nchi jirani.

Ameongeza kuwa “Lakini tunajua ili hayo yafanyike lazima Vijana na watoto wetu na wananchi kwa ujumla wawe na afya ya kutosha ili waweze kulima na kuzalisha kwa kiasi cha kutosha, lakini wawe na elimu ya kutosha ili waweze kujua wanachokifanya lakini pia kuwe na umeme ili kuwe na usalama, tuweze kufanya kazi zetu kwa usalama, Maji safi na salama- Hii ndio ahadi yetu kwenu wana Kalinzi.”

Aidha, ameeleza pia mpango wake wa kuanza majaribio ya utekelezaji wa bima ya afya kwa wote mara baada ya kuchaguliwa kwenye uchaguzi mkuu ujao, akisema serikali yake itagharamia pia matibabu kwa wananchi wasiokuwa na uwezo wa kulipia bima hizo za afya.

The post Dkt. Samia aahidi kuifanya Kigoma kuwa kitovu cha biashara appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post Bosi Wangu Alitaka Kuniangamiza Kwenye Kazi, Lakini Hatua Niliyopiga Ilimfanya Aniombe Msamaha
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook