

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 12, 2025, amekutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) katika Ikulu ya Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, viongozi wa TUCTA wamempongeza na kumshukuru Rais Samia kwa kutekeleza ahadi alizozitoa, ikiwemo nyongeza ya mishahara, kupandisha madaraja ya watumishi wa umma na kuboresha mazingira ya kazi nchini.
Viongozi hao wamesema hatua hizo zimeongeza ari ya wafanyakazi na kuimarisha ustawi wa maisha yao, huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kusukuma mbele ajenda ya maendeleo ya taifa.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!