
Serikali mkoani Mbeya imeelekeza Jeshi la Polisi kufanya kazi usiku na mchana ili wahusika wa mauaji ya Shyrose Mahande, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu cha Mzumbe Ndaki ya Mbeya, wapatikane na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Mkoa wa Mbeya, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Solomon Itunda, amelitaja tukio hilo kuwa la kinyama na haliwezi kufumbiwa macho, huku akisisitiza kuwa wahalifu wote watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Serikali inasisitiza kuwa usalama wa wananchi, hasa wa wanafunzi, ni kipaumbele chake na haitavumilia vitendo vya uhalifu kama hivyo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!