Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mahakama Kuu yatupilia mbali pingamizi la Lissu dhidi ya mashahidi wa siri – Video

  • 5
Scroll Down To Discover

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo Jumanne Agosti 12, 2025, imetupilia mbali maombi ya upande wa utetezi wa Tundu Lissu katika kesi ya marejeo (judicial review) iliyolenga kupinga matumizi ya mashahidi wa siri kama ilivyoombwa na upande wa Jamhuri.

Katika kesi ya msingi inayosikilizwa katika Mahakama ya Kisutu, Lissu anakabiliwa na shtaka la kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni. Jamhuri iliwasilisha ombi la kutumiwa kwa mashahidi wa siri, likidai usalama na masilahi ya mashahidi hao.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Elizabeth Mkwizu. Baada ya kusikiliza shauri hilo, mmoja wa mawakili wa Lissu, Dkt. Rugemeleza Nshala, aliwaambia wanahabari kuwa hawajaridhishwa na uamuzi huo, wakieleza kuwa hatua hiyo “inapoka haki ya mshtakiwa” kwa kumnyima fursa ya kuwajua na kuwakabili mashahidi dhidi yake.



Prev Post Rais Samia akutana na viongozi wa TUCTA Ikulu ya Dar
Next Post CHAUMMA Yapokea Fomu za Uteuzi wa Mgombea Urais
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook