
Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) na Katibu Mkuu wa chama hicho, Salum Mwalimu, amesema hatashiriki katika malumbano na watu wanaomkosoa au kumbeza kuhusu uamuzi wake wa kugombea Urais na kushindana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu ya kuwania Urais katika Ofisi za Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Jijini Dodoma alipoulizwa na wanahabari kuhusu kauli za kumbeza zilizotolewa na Kada wa CCM na aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, Mwalimu amesema haijawahi kuwa tabia yake kujibizana na mtu yeyote.
“Ameyasema ayaseme tu, mimi siko hapa kujibishana na mtu yeyote, haijawahi kuwa hulka yangu, sijawahi kujibishana na mtu wala kumbeza mtu. Acha waseme, ninaamini katika uhuru wa maoni. Sio leo tu, hata nitakapoingia madarakani watu watasema na kusema, lakini mimi nimejikita kwenye nini Watanzania wanataka,” amesema.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!