Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

BENKI YA NMB YAKUTAKA NA WAFANYABIASHARA WAKUBWA JIJINI MWANZA

  • 41
Scroll Down To Discover

NA Mwandishi wetu Mwanza.

Benki ya NMB imeendelea kuonesha dhamira ya dhati katika kuwa mshirika imara wa wafanyabiashara nchini, baada ya kukutana na wafanyabiashara wakubwa 120 wa Mkoa wa Mwanza katika hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika Agosti 1, 2025, jijini Mwanza.

Mkutano huo uliolenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya benki hiyo na wateja wake wakubwa, uliwakutanisha viongozi waandamizi wa NMB, wawakilishi wa serikali pamoja na viongozi wa wafanyabiashara wa jiji hilo, ambapo maoni na matarajio ya pande zote yalitolewa kwa uwazi

Akizungumza na wafanyabiashara katika hafla hiyo, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alieleza uwezo mkubwa wa benki hiyo katika kuhudumia wafanyabiashara nchini, akisema NMB ina uwezo wa kutoa mkopo wa hadi zaidi ya Shilingi bilioni 550 kwa mteja mmoja.

“Hii ni ishara tosha ya uimara wa NMB katika masuala ya kifedha na uwezo wa kweli wa kuwahudumia wafanyabiashara wakubwa,” alisema Mponzi.

Aliipongeza serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara, jambo alilosema limechangia ukuaji wa sekta binafsi na kuongeza uhitaji wa huduma za kifedha

Mponzi alisisitiza kuwa NMB iko tayari kutoa suluhisho mbalimbali kwa wafanyabiashara ikiwemo mikopo, mifumo ya malipo ya kisasa, na huduma za bima.

“Tuna masuluhisho yote muhimu kwa wafanyabiashara. Tumejipanga vizuri kuwahudumia kuanzia mikopo, ubunifu wa malipo hadi bima ya mkono wa pole hivyo sisite kuleta mahitaji yenu, sisi tupo kwa ajili yenu. “alisema Mponzi

Akielezea mafanikio ya benki hiyo, Mponzi alitaja kutambuliwa kwa NMB kama benki salama zaidi nchini kwa miaka mitatu mfululizo na jarida la Global Banking & Finance, pamoja na kushinda tuzo ya benki bora Tanzania mara 11 katika miaka 13 iliyopita kutoka jarida la Euromoney.

Kwa upande wa wafanyabiashara, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Mwanza, Gabriel Mgini, alitoa shukrani kwa NMB kwa uaminifu na mshikamano waliouonesha kwa wateja wao, hata katika nyakati ngumu za biashara.

“Kwa niaba ya wafanyabiashara wenzangu, tunawashukuru sana kwa namna ambavyo mmekuwa karibu nasi. Mmekuwa mstari wa mbele kutuvumilia, kutusikiliza na kutembea nasi katika hatua zote za kibiashara kwenye mafanikio na changamoto,” alisema Mgini na kuongeza

“Ni wazi kuwa kwa mfanyabiashara ili apige hatua, lazima ashirikiane na benki imara. NMB imejidhihirisha kuwa ndiyo benki sahihi kwetu licha ya uwepo wa benki nyingi nchini, huduma za NMB zimeendelea kuwa bora na za kuaminika.”

Mgini aliahidi kuwa wafanyabiashara wa mkoa wa Mwanza wataendelea kuitumia benki ya NMB kama mshirika wao wa karibu katika kukuza biashara, kwa sababu ya huduma bora na ushirikiano madhubuti unaoendelea kuimarishwa kila siku

Katika hafla hiyo, Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Bi. Faraja Ngingo, alisema kuwa wafanyabiashara ni sehemu muhimu katika mafanikio ya benki hiyo na kwamba benki haiwezi kufikia malengo yake bila kuwahusisha wateja wake kwa karibu.

“Tunatambua mchango wenu kwetu, kwani benki yetu haiwezi kufanikiwa bila ninyi kuwepo. Huduma yetu haiwezi kuwa ya thamani bila kuzingatia mahitaji yenu na kujitolea kwenu katika kuwahudumia,” alisema Faraja na kuongeza

“Tunawashukuru kwa kuendelea kutuamini, kwa pamoja tutaendelea kujenga huduma zinazozingatia ubunifu, urahisi, unafuu na maadili. Tunathamini sana imani yenu, uaminifu na mchango wenu katika mafanikio yetu kama benki ya NMB.”

Aliongeza kuwa: “Tutaendelea kujitolea kwa ajili yenu na tunatazamia kuwa na uhusiano wa muda mrefu unaojengwa katika msingi wa kuheshimiana na kushirikiana.”



Prev Post Kailima Awataka Wanahabari Kuhakikisha Usawa kwa Vyama Wakati wa Kampeni
Next Post Mjumbe wa Marekani azuru Gaza huku maelfu wakiendelea kukabiliana na njaa. Katika Dira ya Dunia TV
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook