Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Ng’wasi, Jesca Magufuli Wapata Nafasi ya Uwawakilishi wa Vijana Bungeni – Video

  • 39
Scroll Down To Discover

Msimamizi wa uchaguzi wa Viti Maalum kupitia kundi la UVCCM Bara na Zanzibar watakaowakilisha Vijana kwenye Bunge la Tanzania, leo asubuhi ya August 2 2025, ametangaza matokeo ya kura zilizopigwa usiku wa kuamkia leo ambapo kwa Tanzania Bara wamepatikana Wagombea sita.

1. NG’WASI KAMANI – KURA 409
2. JESCA MAGUFULI – KURA 391
3. HALIMA BULEMBO – KURA 320
4. LULU MWACHA – KURA 316
5. JULIANA MASABURI – KURA 282
6. TIMIDA MPOKI – KURA 280.

Jumla ya Wagombea walikuwa ni 48 (Tanzania Bara 31 na Zanzibar 17) na Wagombea hao 10 (sita wa Bara na wanne wa Zanzibar ) ndio walioshinda baada ya kupata kura za juu zaidi kuliko wengine ambapo kwa upande wa kura zilizopigwa Tanzania Bara jumla ni kura 2466 (Kura zilizoharibika ni 12 na kura halali 2454), na Zanzibar zimepigwa kura 1652 (zimeharibika kura 8 na kura halali 1644).



Prev Post Rais Ruto Amkaribisha Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta Ikulu ya Nairobi
Next Post SBL Yazindua Mpango wa Kilimo Biashara Kuongeza Mavuno kwa Wakulima
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook