Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Ruto Amkaribisha Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta Ikulu ya Nairobi

  • 49
Scroll Down To Discover

Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. William Samoei Ruto, amemkaribisha Rais mstaafu wa taifa hilo, Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta, katika Ikulu ya Nairobi na kumtembeza rasmi katika majengo hayo yenye sura mpya, mara baada ya kuhitimika kwa mkutano muhimu wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuhusu juhudi za kurejesha amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Katika taarifa yake, Rais Ruto alieleza kuwa mkutano huo wa pamoja wa viongozi wa Kiafrika umejadili kwa kina mbinu za pamoja za kuimarisha amani na uthabiti katika ukanda wa DRC Mashariki, akisisitiza kuwa juhudi hizo hazipingani na zile za kimataifa kama za Doha na Washington, bali zinajenga msingi imara wa suluhisho la Kiafrika kwa changamoto za Kiafrika.

“Nimepata nafasi ya kipekee ya kumtembeza rafiki yangu wa muda mrefu, Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, kuzunguka Ikulu ya Nairobi mara baada ya mkutano wa pamoja wa EAC na SADC kuhusu kurejesha amani na uthabiti katika DRC Mashariki,” alisema Rais Ruto.

Ziara hiyo ya kipekee imeonesha mshikamano kati ya viongozi wa sasa na wa zamani nchini Kenya, ikiwa ni ishara ya umoja wa kitaifa na mshikamano wa kidiplomasia, hususan katika wakati ambapo bara la Afrika linahitaji sauti moja katika kuzipatia suluhisho changamoto za kiusalama na maendeleo.



Prev Post Shule ya Sekondari ya Makongo Yaweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Bohari
Next Post Ng’wasi, Jesca Magufuli Wapata Nafasi ya Uwawakilishi wa Vijana Bungeni – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook