Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Brigitte Macron Apambana na ‘Uongo wa Mtandaoni’ Katika Mahakama ya Marekani

  • 4
Scroll Down To Discover

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mkewe Brigitte Macron wamefungua kesi ya madai ya kashfa dhidi ya Mwanaharakati kutoka Marekani, Candace Owens kwa madai ya kusambaza uvumi kwamba Mama Brigitte alizaliwa akiwa Mwanaume.

Kesi hiyo iliwasilishwa jana Jumatano katika jimbo la Delaware, Marekani, ikieleza kuwa Owens amekuwa akieneza taarifa hizo za kufikirika na za kufedhehesha kuhusu Mama Macron.

Owens, ambaye ana mamilioni ya wafuasi katika mitandao ya kijamii na anaendesha Podikasti maarufu, amekuwa akirudia mara kwa mara madai hayo, mnamo Machi 2024, alisema yuko tayari kuweka sifa yake ya kitaaluma rehani kwa imani yake kuwa Bi Brigitte ni mwanaume.

Katika kipindi kipya cha Podikasti yake kilichotolewa jana Jumatano, Owens alisisitiza msimamo wake na kuipuuza kesi hiyo, alimdhalilisha Mama Macron na kusema kuwa kesi hiyo ni mbinu ya wazi na ya kukata tamaa na kutafuta huruma ya umma.

Tuhuma hizo, ambazo zimekuwa zikisambaa mtandaoni kwa miaka kadhaa, zinadai kimakosa kwamba Mama Brigitte alizaliwa mwanaume kwa jina la Jean-Michel Trogneux jina la kaka yake wa damu.

Owens amekuwa akieneza madai hayo kwa hadhira yake, ikiwa ni pamoja na wafuasi wake wapatao milioni 7 kwenye mtandao wa X na mapema mwaka huu, alichapisha mfululizo wa video uliopewa jina “Becoming Brigitte”.

Katika taarifa iliyotolewa na Wanasheria wa Familia ya Macron, walisema kuwa walijaribu mara kadhaa kumuomba Owens abadili kauli yake, lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda.



Prev Post Tammy Slaton Ashtua Dunia kwa Mwonekano Mpya Baada ya Kupunguza Uzito
Next Post JK Kinara Maandalizi Ya Kongamano La TICAD 9 Nchini Japan
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook