
Mwigizaji maarufu wa Marekani, Tammy Slaton, ameacha mashabiki wake midomo wazi baada ya kuonesha mabadiliko makubwa ya mwonekano kufuatia safari ya miaka minne ya kupunguza uzito.
Tammy, ambaye hapo awali alikuwa na uzito wa zaidi ya kilo 325, sasa ameshuka hadi kilo 91. Mabadiliko haya yamechangiwa na lishe maalum, mazoezi ya mwili pamoja na upasuaji wa kupunguza uzito.
Mashabiki wake wengi wameonyesha mshangao na furaha, wakimpongeza kwa juhudi alizoweka na kuamini kuwa haonekani tena kama alivyoonekana hapo awali. Tammy amesema kuwa safari hiyo haikuwa rahisi, lakini ilikuwa muhimu si tu kwa ajili ya kupunguza uzito, bali pia kwa kujipenda, kupata afya bora, na kuboresha maisha yake kwa ujumla.
Miongoni mwa sababu kubwa zilizopelekea kufanya maamuzi hayo ni tukio la karibu lililowahi kumtokea la kunusurika kumpoteza maisha alipokimbizwa hospitalini mara baada ya kushindwa kupumua, ambapo madaktari walimueleza kuwa alikuwa kwenye hatua ya hatari ya kupoteza maisha.
Tukio hilo lilimfumbua macho na kumfanya afikirie upya juu ya afya ya maisha yake.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!