Uwanja huo wa ndege, ambao ndio wenye shughuli nyingi zaidi nchini Uingereza, umeonya kuhusu "usumbufu mkubwa" katika siku zijazo na kuwaambia abiria wasisafiri "kwa hali yoyote" hadi utakapofunguliwa tena.
"Ili kudumisha usalama wa abiria wetu na wenzetu, hatuna chaguo ila kufunga Heathrow hadi 23:59 mnamo Machi 21, 2025," msemaji alisema.
"Tunajua hili litakatisha tamaa abiria lakini tunataka kuwahakikishia kuwa tunafanya bidii iwezekanavyo kutatua hali hiyo," waliongeza.
"Huku wafanyakazi wa zimamoto wakishughulikia tukio hilo, hatuna uwazi kuhusu ni lini nguvu za umeme zinaweza kurejeshwa kwa uhakika," msemaji wa Heathrow alisema.Uwanja huo wa ndege umeomba radhi kwa usumbufu huo na umewashauri abiria kuwasiliana na mashirika yao ya ndege kwa taarifa zaidi.
Heathrow ndio uwanja mkubwa zaidi wa usafiri wa anga nchini Uingereza, ukishughulikia karibu ndege 1,300 zinazotua na kupaa kila siku.
Rekodi ya abiria milioni 83.9 walipitia vituo vyake mwaka jana, kulingana na data yake ya hivi karibuni.
Angalau safari 1,351 za ndege kwenda na kutoka Heathrow zitaathiriwa na hatua hii, tovuti ya ufuatiliaji wa safari za ndege ya Flightradar24 ilisema kwenye X, na baadhi ya ndege 120 zilizoathiriwa tayari ziko angani mapema asubuhi.
Moto katika kituo kidogo cha Hayes, magharibi mwa London, umeacha maelfu ya nyumba bila umeme na kusababisha karibu watu 150 kuhamishwa kutoka katika maeneo yaliyopo na uwanja huo.
Huduma za dharura ziliitwa kwa mara ya kwanza kwenye eneo la tukio saa 23:23 siku ya Alhamisi, na video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha miale ya moto na moshi ukifuka kutoka kwa kituo hicho usiku kucha. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!