Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Putin atavunja makubaliano ya amani na Ukraine yasipolindwa - Uingereza

  • 62
Scroll Down To Discover

Rais wa Urusi, Vladimir Putin, atavunja makubaliano ya amani na Ukraine ikiwa hayatakuwa na ulinzi, amesema Sir Keir Starmer, baada ya kuhudhuria mkutano wa viongozi wakuu wa jeshi mjini London.

Waziri Mkuu wa Uingereza alisema makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano kati ya Urusi na Ukraine yatakuwa ya kudumu tu ikiwa kutakuwa na mipango ya kiusalama.

Alikuwa akizungumza huko Northwood, London, ambapo zaidi ya nchi 20 zilihudhuria mkutano wa faragha kujadili mapendekezo ya kupeleka wanajeshi nchini Ukraine ili kusaidia kuhakikisha usalama wa nchi hiyo kama sehemu ya makubaliano yoyote ya amani.

Sir Keir alisema mipango ya usalama lazima iwe kwa Urusi kuwa kutakuwa na "matokeo makali" ikiwa itavunja makubaliano yoyote.

Waziri Mkuu huyo alisema Uingereza na washirika wake wanapiga hatua kutoka kwenye "msukumo wa kisiasa" hadi "mpango wa kijeshi", ambao alisema lazima ufanyike sasa kabla ya makubaliano kufikiwa.

Alisema: "Ni muhimu sana tufanye kazi hiyo kwa sababu tunajua jambo moja kwa uhakika, nalo ni kuwa makubaliano yasiyo na kitu chochote nyuma yake ni jambo ambalo Putin atavunja. "Tunajua hilo kwa sababu lilitokea hapo awali. Niko wazi kabisa akilini mwangu kuwa litatokea tena."

Sir Keir alikanusha mpango wa kuondoa wanajeshi wa Uingereza kutoka nchi kama Estonia ili kuwapeleka Kyiv,

akisema: "Hakuna kurudi nyuma kuhusu ahadi zetu kwa nchi nyingine."

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, John Healey, alihudhuria mkutano huo wa faragha wa viongozi wa kijeshi kutoka nchi zinazounda kile ambacho Sir Keir ameita "muungano wa wenye nia".

Downing Street ilisema viongozi hao wa kijeshi wangekuwa wakihusika katika "mpango wa kina" wa maelezo ya uwezekano wowote wa kupelekwa kwa wanajeshi Ukraine.

Uingereza iliitisha mkutano wa wakuu wa jeshi baada ya mkutano wa kilele uliofanyika mapema mwezi huu ulioshirikisha nchi 26.



Prev Post Umeme: Uwanja wa ndege nchini Uingereza kufungwa siku nzima leo
Next Post Namibia yamuapisha Rais wake wa kwanza mwanamke
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook