Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Benk Ya NMB Imejizatiti Kutoa Huduma Bora Kwa Walimu

  • 42
Scroll Down To Discover

Na Mwandishi Wetu,Manyara.

Benki ya NMB imesema itaendelea kutoa huduma bora kwa Walimu ikiwemo kuwapatia mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha kujiendeleza kiuchumi na kijamii ili kuhakikisha ustawi wa kundi hilo muhimu kwenye jamii.

Hayo yamesemwa na Meneja mwandamizi Wa wateja Binafsi Wa Beki ya NMB Ally Ngingite wakati akizungumza na walimu Wa wilaya ya Babati Mkoani Manyara Katika Bonanza la Mwalimu Spesho inayoandaliwa na Benki hiyo kila mwaka ambapo amesema wataendelea kutoa mikopo ya haraka kwa walimu ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Mkuu Wa Idara ya Wateja Binafsi Benki ya NMB Aikasia Muro amesema bonanza hilo ambalo linafanyika kwa mwaka wa kumi sasa ni maalum kwa ajili ya kuwakutanisha walimu na kuwapatia masuluhisho ya huduma za kibenki ikiwemo mikopo yenye riba nafuu pamoja na huduma nyingine nyingi ambazo ni rafiki kwa walimu.

Mgeni Rasmi katika Bonanza hilo Kaimu Mkurugenzi Wa Halmashauri ya Mji Babati Gasto Silayo amesema walimu wameendelea kunufaika kupitia benki hiyo na ushirikiano ni mkubwa kati ya benki hiyo na Serikali kutokana na huduma bora wanayotoa kwa wateja wake

Baadhi ya walimu wilayani humo wameishukuru Benki hiyo kwa kuwarahisishia baadhi ya mambo kupitia mikopo wanayotoa kwa walimu hivyo wamewaomba walimu wengine kujiunga na Benki hiyo ili kufaidi matunda yanayopatikana katika benki hiyo kwa kuwaleta watu karibu



Prev Post Majaliwa Amwakilisha Rais Dkt. Samia Ibada Ya Kuwekwa Wakfu Askofu Mteule Dkt. Daniel Mono
Next Post Katibu mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda na Zanzibar Fatma awataka wafanyabiashara kuchangamkia Fursa kati ya China na Tanzania 
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook