
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko ya uongozi kwa kuwahamisha au kuwaweka kando wakuu wa mikoa watano, akiwemo Paul Makonda (Arusha).
Wengine ni Peter Serukamba (Iringa), Thobias Andengenye (Kigoma), Dk. Juma Homera (Mbeya), na Daniel Chongolo (Songwe).
Taarifa hiyo imetolewa usiku wa Juni 23, 2025 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka.
Mabadiliko haya yanakuja zikiwa zimesalia siku nne kabla ya dirisha la uchukuaji na urejeshaji fomu ndani ya CCM kufunguliwa, Juni 28. Duru za kisiasa zinaeleza kuwa baadhi ya waliopumzishwa wanatarajiwa kugombea ubunge kwenye majimbo mbalimbali, akiwemo Makonda (Arusha Mjini), Serukamba (Kigoma Kaskazini), Dk. Homera (Namtumbo), na Chongolo (Makambako).
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!