Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

KUHUSU ISHU YA IBENGE KUJA AZAM FC….UKWELI WOTE HUU HAPA…MABOSI WAFUNGUKA A-Z…

  • 29
Scroll Down To Discover

WAKATI tetesi zikiendelea kumuhusisha Kocha Mkuu wa Al Hilal ya Sudan, Florent Ibenge, na klabu ya Azam FC, uongozi wa timu hiyo umeweka wazi kuwa kocha huyo ni mmoja wa walimu bora barani Afrika ambaye timu yoyote ingejiweka kwenye nafasi nzuri kwa kuwa naye.

Ibenge ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, anatajwa kuwa kwenye mazungumzo na Azam FC kuchukua mikoba ya Kocha Rachid Taoussi ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Ibenge ana uzoefu mkubwa kwenye soka la Afrika akiwa tayari ameinoa AS Vita Club na timu ya taifa ya DR Congo kabla ya kujiunga na Al Hilal ya Sudan.

Msemaji wa Azam FC, Hashim Ibwe, amesema kwa sasa klabu hiyo inaendelea na programu zake za kawaida chini ya Kocha Rachid, huku akieleza kuwa suala la mkataba wa mwalimu huyo bado liko mezani kwa viongozi wakuu wa klabu hiyo.

“Tuna mechi Jumatano Juni 18, nyumbani dhidi ya Tabora United. Kocha Rachid bado anafanya kazi yake kwa weledi mkubwa na tunamheshimu kwa mchango wake. Kuhusu kuongeza mkataba, hilo ni suala ambalo lipo mikononi mwa viongozi wa juu wa klabu na watafanya tathmini kabla ya kufanya maamuzi,” amesema Ibwe.

Hata hivyo, Ibwe hakusita kumpa sifa Ibenge kwa uwezo wake wa kufundisha na kuandaa timu zenye ushindani barani Afrika.

Ameeleza kuwa ujio wake Tanzania unaweza kuleta chachu mpya katika soka la ndani kwa kuibua vipaji na kuongeza ushindani.

“Kwa upande wangu, Ibenge ni mwalimu mzuri sana. Kila timu Afrika inahitaji kuwa naye. Ni mtu anayejua kazi na ana uwezo mkubwa wa kuwapa maadili na nidhamu wachezaji, hasa vijana. Naamini hata Watanzania wangependa kumuona akiifundisha timu ya hapa nchini,” amesema.

Mpaka sasa, uongozi wa Azam FC haujatoa kauli rasmi kuhusu mustakabali wa benchi la ufundi kwa msimu ujao, lakini taarifa za ndani zinaeleza kuwa utafiti na mazungumzo na makocha mbalimbali yanaendelea ili kuhakikisha timu inakuwa na benchi la ushindani kuelekea msimu wa 2025/26.

Florent Ibenge ana sifa ya kuifikisha AS Vita kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2014, pia kuiongoza DR Congo kutwaa medali ya shaba katika michuano ya AFCON mwaka 2015 – jambo linalomfanya kuwa mmoja wa makocha wenye heshima kubwa Afrika.

The post KUHUSU ISHU YA IBENGE KUJA AZAM FC….UKWELI WOTE HUU HAPA…MABOSI WAFUNGUKA A-Z… appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post CAMARA KUPEWA THANK YOU SIMBA???…..MABOSI WATOFAUTIANA MKATABA MPYA….
Next Post ZIMBWE JR KIMEEELEWEKA SIMBA SC….ISHU YA NGOMA KUSALIA MHHHHH….
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook