IMEELEZWA kuwa uongozi wa klabu ya Simba upo katika mazungumzo ya kumuongeza mkataba beki wao, Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ kusalia ndani ya klabu hiyo huku kiungo Fabrice Ngoma akijadiliwa kusalia au kutemwa.
Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Simba zimeeleza kuwa Zimbwe Jr anaweza kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo ikiwa ni sehemu ya mazungumzo yanayoendelea hivi sasa kati ya pande zote mbili.
“Kuhusu Ngoma bado ni suala la kujadiliwa maana viongozi ndio wapo wanaangalia kumuongeza mkataba au kumtema. Suala lake bado ni gumu na maamuzi ya mwisho tutajua baada ya ripoti ya Kocha Mkuu Fadlu Davids itakapotufikia,” amesema mmoja wa viongozi wa klabu hiyo.
Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba,Ahmed Ally alisema kwa sasa anachotambua ni kuwa wachezaji ambao kocha Fadlu atawapendekeza katika ripoti yake kusalia, bila shaka watasalia.
“Kwa sasa siwezi kusema kwa uhakika kwa sababu suala hilo lipo kwa benchi la ufundi linaloongozwa na Fadlu. Akitoa mapendekezo ya hao nyota waliomaliza mikataba yao, basi waliopendekezwa kusalia watasalia ndani ya kikosi,” amesema Ahmed.
Ikumbukwe kuwa Zimbwe Jr amekuwa nguzo muhimu katika safu ya ulinzi ya Simba kwa misimu kadhaa na kiwango chake thabiti kimewafanya mashabiki wengi kutaka aongezewe mkataba, tofauti na hali ya sintofahamu inayoendelea kumkumba Ngoma ambaye amekuwa na wakati mgumu kuonyesha makali yake msimu huu.
The post ZIMBWE JR KIMEEELEWEKA SIMBA SC….ISHU YA NGOMA KUSALIA MHHHHH…. appeared first on Soka La Bongo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!