MOUSA Camara kipa namba moja wa Simba SC anatajwa kuwa kwenye hesabu za kukutana na Thank You ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu,Fadlu Davids.
Camara ni chaguo la kwanza ndani ya Simba SC ambayo ipo kwenye maandalizi kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KenGold unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Juni 18.
Taarifa zinaeleza kuwa kipa huyo ambaye amekaa langoni kwenye mechi 25 za ligi akikusanya hati safi 17 akiwa ni kinara kwa makipa ambao hawajafungwa mechi nyingi kiwango chake bado hakijawafurahisha mabosi wa timu hiyo kutokana na makosa ambayo amekuwa akiyafanya.
Kumekuwa na mgawanyiko ndani ya uongozi wa Simba SC ambapo wapo ambao wanahitaji kipa huyo asepe na wengine wanaamini akipata muda atakuwa bora zaidi.
Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union mzunguko wa kwanza, Camara alifungwa mabao mawili kutokana na makosa ya safu ya ulinzi na makosa yake kwa kutokuwa kwenye eneo lake mara zote na mchezo dhidi ya Yanga SC alifanya kosa katika kuokoa mpira ambao haukuwa na hatari dakika za lala salama na mwisho akafungwa bao 1-0.
Makosa ambayo kafanya yanatajwa kumuhukumu huku baadhi ya viongozi wakibainisha kwamba kipa huyo alikuwa langoni kwenye mechi za kimataifa mpaka timu inatinga hatua ya fainali.
The post CAMARA KUPEWA THANK YOU SIMBA???…..MABOSI WATOFAUTIANA MKATABA MPYA…. appeared first on Soka La Bongo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!