

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali na kuwapangia vituo vya kazi, kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka.
Katika uteuzi huo, Rais Samia amemteua Dkt. Delilah Charles Kimambo kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, akichukua nafasi ya Prof. Mohamed Janabi ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika.
Wengine walioteuliwa na Rais Samia ni:
Jaji Mstaafu Hamisa Hamis Kalombola aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma kwa kipindi cha pili, Paul Thomas Sang’awa aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa SELF kwa kipindi cha pili na Jaji Rose Ally Ebrahim aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal).
Pia Rais Samia amempangia kituo cha kazi Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk aliyepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!