

Chama Cha Mapinduzi kusisitiza kwakuwa Sheria halali za nchi zipo, zitamkabili mtu yoyote , kikundi na watu wenye ndoto za kufanya ushawishi wa kupandikiza Siasa za Ubaguzi, Ukabila na Udini.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis, ameeleza hayo huku akisema mikono ya sheria ianze kuwatia mbaroni wale wote wenye kusudio hilo .
Mbeto alisema Sheria ni msumeno hivyo mtu au watu wanaofikiri wanaweza kufanikisha mradi hatari wa kuwagawa wananchi , waangukiwe na mkono wa Sheria.
Alisema kwa uzoefu utokanao na hatari iliozikumba nchi kadhaa kutokana na uchochezi wa ukabila ,ubaguzi na udini , na matokeo yake yameleta madhara na maafa hivyo yasiachwe yachipue, yakue na kustawi .
“Kuna baadhi ya Wanasiasa aidha kutokana na kufilisika kwao kisiasa, wakianza kutumia lugha za Ubaguzi, Udini na Ukabila wadhibitiwe . Sheria zipo hivyo zisimwache mtu atambe mitaani “Alisema Mbeto .
Katibu huyo Mwenezi alisema kuna maadui watatu Ujinga , Umasikini na Maradhi, lakini pia maadui wa usalama wa Taifa na Amani yetu ni Udini, Ukabila na Ubaguzi.
“Vyama vyote vya Siasa vina sera zake. Program za kisiasa na kioganaizesheni. Ikiwa vipo vyama havina sera viache Siasa .Kutumia ukabila, udini na Ubaguzi katika Siasa ni kwenda kinyume na Sheria “Alieleza
Aidha, Katibu Mwenezi huyo alisema Sheria ya Usajili wa Vyama Vya Siasa Namba 5 ya Mwaka 1992, inakataza matumizi ya siasa za Ubaguzi, Udini na Ukabila katika Uwanja wa kufanyia Siasa.
Mbeto aliongeza kusema endapo sheria zinazopiga marufuku mambo hayo hatari kwa taifa ,ikiwa zitakaa kimya ,kadri siku zinavyokwenda mbele , itaonekana masuala hayo ni mambo ya kawaida .
“Hivi sasa kuna baadhi ya Vyama vy Siasa Uongozi wote wa juu umeshikwa aidha na viongozi wa dini moja. Baya zaidi ukakuta wanatoka kanda moja pia si ajabu wakawa kabila moja” Alisistiza Katibu huyo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!