
Watu 09 wamefaniki na wengine 44 kujerubiwa katika ajali ilyotokea majira ya Alfajiri eneo la Lugono Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Barabara Kuu ya Morogoro-Iringa baada ya gari aina ya Scania yenye Namba za usajil T.406 CZS yenye Tela namba T. 804 BUB kugongana na Basi la Abiria Higer Ecpress T.523 EKM. likitokea Mbeya kuelekea Dar es salaam.
Ajali hii ambayo imehusisha gari liliobeba Shehena ya Sukari na Basi la Abiria liilokuwa likitokea Jijini Mbeya kuekelea Dar es salaami na kusababisha watu 09 kufanki papo hapo, watu 44 wakijeruhiwa katika ajali hiyo wakiwamo watu wazima 37 na watoto 07.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mandamizi wa Jeshi la Polisi Alex Mkama amesema Jeshi hilo linamtafuta Dereva wa gari la Mizigo ambalo limehusika katika ajali hoyo, ambapo uchunguzi wa awali umebaini kuwa dereva huyo alishindwa kudhibiti gari lake na kupoteza mwelekeo, akitoa wito pia kwa madereva kuzingatia na kufuata sheria za usalama barabarani.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!