
Rais wa Jamhuri ya Kenya William Ruto amesema Jumatano kuwa kifo cha mwanablogu aliyekuwa kizuizini polisi kilitokea mikononi mwa polisi, na kuwaomba Wakenya wawe na subira wakati uchunguzi ukiendelea.
Kifo cha Albert Ojwang kimekuwa tukio la hivi punde zaidi kuchunguzwa na idara za usalama za Kenya baada ya miaka mingi ya mauaji ya kiholela na kutoweka kwa watu ambao Ruto ambapo amekuwa akiahidi kukomesha vitendo hivyo mara kwa mara licha ya hasira ya umma inayoongezeka.
Awali Polisi walisema Ojwang, 31, alikamatwa magharibi mwa Kenya siku ya Ijumaa kwa madai ya kumkashifu naibu mkuu wa polisi nchini humo mtandaoni, na alifariki baada ya kugonga kichwa chake kwenye ukuta wa mahabusu.

Hata hivyo akiwa mbele ya kikao cha baraza la Seneti kuhusu mauaji ya Ojwang, Inspekta Mkuu wa Polisi nchini humo Inspekta Jenerali Douglas Kanja ameomba radhi mbele ya bunge la Seneti kwa niaba ya polisi ya taifa kwa kutoa ripoti isiyo sahihi kuhusu uchunguzi wa mauaji ya mwanablogi mwenye ushawishi Albert Ojwang.
Majeraha yake, ikiwa ni pamoja na jeraha la kichwa, shingo na uharibifu wa mwili, yalionesha kuwa shambulio lilikuwa sababu ya kifo chake, kulingana na mchunguzi maiti wa serikali , Bernard Midia, ambaye alikuwa sehemu ya timu iliyofanya uchunguzi wa maiti.
Kifo cha Ojwang, ambaye aliandika kuhusu masuala ya kisiasa na kijamii, kimezua shutuma nyingi kutoka kwa makundi ya kutetea haki za binadamu na kusababisha maandamano nje ya chumba cha kuhifadhia maiti ambapo mwili wake ulifanyiwa uchunguzi katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Na Elvan Stambuli GPL.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!