
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadu Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema uchaguzi utafanyika kwa mujubu wa katiba na sheria kama ilivyopangwa, hivyo hata wakichapisha na kutuma ‘No Reform No Election’ mara milioni haisaidii.
Pia amesema kinachoweza kusababisha uchaguzi kuahirishwa au kusogezwa mbele ni vita lakini Tanzania hakuna vita, hivyo maneno hayo yanayochapishwa kwenye mitandao hayasaidii uchaguzi upo palepale.
Makalla ameeleza hayo Juni 8,2025 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja Manyema Wilaya ya Moshi Mjini Mkoani Moshi akiendelea na ziara yake ya mikoa mitatu ya Kanda ya Kaskazini ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
Akizungumza kujibu sekeseke linaloendelea katika mitandao ya kijamii mwishoni mwa wiki iliyopita Makalla amesema machapisho yanayochapishwa yakiandikwa ‘No reform no election’ hayana maana yoyote na haiwezi kuwa sababu ya kuahirishwa kwa uchaguzi.
Amesema sabbau kubwa inayopelekea uchaguzi kuahirishwa au kusogezwa mbele ni kuwa na vita lakini Tanzani ahakuna vita na ni nchi ya amani akiwasisitiza wananchi kuitunza amani hiyo iliyopo sasa, wakati na hata baada ya uchaguzi.
“Kwahiyo hata yale yanayoendela kwenye mitandao hata wakichapisha machapisho mamilioni na mamilioni ya ‘No Reform no election’ uchaguzi upo pale pale haisaidii we njoo tu weka pale chapisho haisaidii, hiyo ni nadharia kujifurahisha Uchaguzi upo palepale,”
Makalla amesema mabadiliko lukuki yamefanyika katika sheria ya uchaguzi kwa kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi, lakini mabadiliko ya katiba nzima yanahusisha makundi mbalimbali.
Makalla amesema katiba kwa ujumla inahusisha makundi mbalimbali kwa sababu ni jambo kubwa kwani inahusu haki za kina mama, watoto, wafanyakazi na makundi mengine lakini wao wanajali mambo yatakayowaingia madarakani tu.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!