Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mashabiki Wa PSG Waunga Mkono Palestina Katika Mechi Ya Fainali Ya Klabu Bingwa Ulaya

  • 46
Scroll Down To Discover


Mashabiki wa PSG waunga mkono Palestina katika mechi ya fainali ya klabu bingwa Ulaya
Mashabiki wa timu ya soka ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa wametangaza himaya na uungaji mkono wao kwa Palestina.

Katika mechi ya jana ya fainali ya klabu bingwa barani Ulaya iliyochezwa katika Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich, Ujerumani, mashabiki wa timu hiyo walikuwa na bendera kubwa ya Palestina na maberamu yaliyokuwa na maandishi ya kuunga mkono Palestina.

Mashabiki wa Paris Saint-Germain wakiwa katika Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich, walilaani vikali vitendo vya kikatili vya utawala ghasibu wa Kizayuni na kushikilia bendera ya kuiunga mkono Palestina. Beramu kubwa lililokuwa limebebwa na mashabiki wa PSG lilisomeka: “Komesheni mauaji ya kimbari huko Gaza.”

Klabu ya PSG ilitwaa kwa mara ya kwanza katika historia yake kombe la klabu bingwa barani Ulaya katika fainali hiyo ya jana baada ya kuitandika Inter Milan ya Italia mabao matano kwa bila.

Himaya na uungaji mkono kwa Palestina umeongezeka mno katika mashindano mbalimbali ya michezo katika miezi ya hivi karibuni huku Israel ikitengwa na kukosolewa vikali kutokana na jinai zake dhidi ya Wapalestina.

Hivi karibuni pia, wakaazi wa mji mkuu wa Uhispania Madrid waliandamana wakipinga kuingia mjini humo timu ya mpira wa kikapu ya Maccabi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unatenda jinai dhidi ya Wapalestina.

 



Prev Post Idadi ya waliofariki dunia Nigeria yafikia 200
Next Post Wiki ya AZAKI 2025 Kuanza na Mjadala Kuhusu Dira ya Maendeleo 2050
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook