Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Trump Azitaka Kampuni za US Zitengeneze Droni Kama za Iran

  • 31
Scroll Down To Discover

 

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema ameziomba kampuni za Marekani kutengeneza ndege zisizo na rubani zinazofanana na droni za Iran, ambazo si ghali sana bali zina kasi ya juu na hatari.

Trump aliyasema hayo nchini Qatar jana Alhamisi kabla ya kuelekea Umoja wa Falme za Kiarabu kwa duru ya tatu na ya mwisho ya ziara yake iliyoanzia nchini Saudi Arabia mapema wiki hii.

Trump amesema, “Niliiambia moja ya kampuni za ulinzi kwamba nahitaji ndege nyingi zisizo na rubani, na unajua, Iran inatengeneza droni nzuri, na wanazitengeneza kwa gharama ya dola 35,000 hadi 40,000.”

Ameeleza kuwa, “Kwa hiyo niliiambia kampuni hiyo, ‘Nataka kuona kitu kama hicho.’ Wiki mbili baadaye, walinijia na ndege isiyo na rubani ambayo iligharimu dola milioni 41! Nikasema, ‘Sivyo nilivyokuwa nikizungumza. Milioni arobaini na moja? Ninazungumza juu ya kitu ambacho kinagharimu dola 35,000 hadi dola 40,000, ili tuweze kuzirusha kwa maelfu.”

Maendeleo makubwa na ya kasi ya Iran katika teknolojia ya ndege zisizo na rubani na uwezo wake wa kufanya mashambulizi ya masafa marefu katika vita vya droni kwa usahihi wa hali ya juu kumeimarisha nguvu za kijeshi za nchi hii katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Mpango wa kisasa wa ndege zisizo na rubani wa Iran umekuwa miongoni mwa mafanikio ya jeshi la taifa hili katika kutengeneza vifaa vya asili vya kujihami ili kufanya vikosi vya jeshi lake kujitosheleza, mkabala wa vitisho na vikwazo vya miaka mingi vya Wamarekani.

Stori na Elvan Stambuli, GPL

WASTARA AWEKEWA SUMU KWENYE SODA – ALIA – ANAOGOPA KUFARIKI KAMA CARINA- TUMBO LIMEVIMBA – INI JEUSI



Prev Post PIGA MSHINDO LEO HII KWA KUPITA NA ODDS HIZI KALI KUTOKA MERIDIANBET…
Next Post MAGAZETI ya Leo Jumapili tarehe 18 May 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook