
MAGAZETI ya Leo Jumapili tarehe 18 May 2025
MAGAZETI ya Leo Jumapili tarehe 18 May 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema mwaka huu atapiga kura Chamwino mkoani Dodoma, badala ya Zanzibar kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Akizungumza baada ya kuboresha taarifa zake za mpiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura leo Jumamosi, Mei 17, 2025, Chamwino, Rais Samia amesema: “Ndugu zangu, nami nimeona nijiunge nanyi hapa kituoni kwetu… Huko nyuma nilikuwa napiga kura Zanzibar kwa sababu nilikuwa Makamu wa Rais… lakini mwaka huu inabidi nipige kura hapa Makao Makuu ya nchi, ambako ndiko yalipo makao ya Serikali.”
Amesema licha ya kuwa mkazi wa Chamwino kwa muda mrefu na kupiga kura huko mara nyingi, alilazimika kupiga kura Zanzibar alipokuwa Makamu wa Rais. Hata hivyo, kwa sasa, akiwa Rais, ameamua kurekebisha taarifa zake ili kupiga kura Chamwino.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!