Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Makalla: CCM Itaendelea Kutatua Kero za Wananchi

  • 32
Scroll Down To Discover

•Aongea na wananchi DUMILA na kusikiliza kero

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi(CCM) CPA, Amos Makalla amesema chama hicho, ndicho chenye jukumu la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili Watanzania..

CPA, Makalla amesema wajibu huo unatekelezwa vema na CCM, akiwataka Watanzania kutokuwa na wasiwasi kuhusu utatuzi wa kero zinazowakabili kwa sababu maendeleo yanaendana na changamoto.

CPA, Makalla ameeleza hayo leo katika Kata ya Dumila wilayani Kilosa aliposimama kuwasalimia wananchi wa eneo akieleke wilayani Gairo kufanya mkutano wa hadhara.

“CCM ndio yenye thamana ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wengine hawawezi hilo,” amesema CPA.

Katika mkutano huo, Makalla alizibeba kero za maji, barabara, ushuru na stakabadhi gharani zilizowasilishwa na wananchi wa Dumila aliyewapa fursa ya kueleza changamoto zinazowakabili.



Prev Post Serikali Itaendelea Kutoa Mikopo Kwa Vikundi Vya Wanawake
Next Post Dkt. Philip Mpango Azitaka Benki Tanzania Kuimarisha Usalama wa Fedha na Teknolojia
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook