Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Trump wa Marekani awasili Saudia, alenga kuto kitita cha dola trilioni 1

  • 3
Scroll Down To Discover

Rais wa Marekani, Donald Trump, amewasili mjini Riyadh katika awamu ya kwanza ya ziara yake ya siku nne katika eneo la Asia Magharibi, ambapo analenga kupata hadi dola trilioni moja za uwekezaji kutoka Saudi Arabia.

Trump alipokelewa na Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Khalid, jijini Riyadh,juzi Jumanne.
Saudi Arabia ni kituo cha kwanza cha ziara yake ya kimataifa tangu aanze muhula wake wa pili kama rais wa Marekani.

Ripoti zinaeleza kuwa Trump anatarajiwa kusaini mikataba ya thamani ya zaidi ya dola trilioni moja wakati wa ziara yake katika taifa hilo la Ghuba ya Uajemi ambalo ni tajiri kwa mafuta.

Duru zinadokeza kuwa makubaliano hayo yanajumuisha uwekezaji katika makampuni ya teknolojia ya akili mnemba, uzalishaji wa nishati, pamoja na ununuzi wa silaha kutoka kwa watengenezaji wa zana za kijeshi wa Marekani.

Ripoti za awali zimedokeza kuwa Marekani haishinikizi tena Saudi Arabia kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel kama sharti la kuendeleza mazungumzo ya ushirikiano wa nyuklia na ufalme huo.

Mnamo mwaka 2017, Trump alichagua Saudi Arabia kama nchi yake ya kwanza kuitembelea akiwa rais, ambapo alipata ahadi ya uwekezaji wa zaidi ya dola bilioni 450 kwa ajili ya uchumi wa Marekani.

Stori na Elvan Stambuli, GPL

AUAWA KWA RISASI AKIWA MOJA KWA MOJA TIKTOK NDANI ya SALUNI – UCHUNGUZI UNAENDELEA



Prev Post Mfalme Zumaridi Akamatwa Na Polisi, Aliwaambia Watoto ‘Yeye Ni Mungu’ Anaweza Kuwatenganisha Na Kifo – Video
Next Post Selcom Yazindua Rasmi Vituo 10 vya Huduma kwa Wateja
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook