
Kupitia vituo hivi, mawakala wa Selcom sasa wana uwezo wa kupata float kwa urahisi zaidi kuliko awali, jambo linalowawezesha kutoa huduma kwa ufanisi. Wakati huo huo, wateja wa Selcom Pesa wanaweza kufika katika vituo hivyo kuongeza pesa kwenye akaunti zao papo hapo, kupata kadi ya Mastercard, na kupewa msaada wa moja kwa moja kuhusu matumizi ya huduma za nyingi zilizopo kwenye Selcom Pesa.
Vituo vya Selcom Experience Centers vinapatikana katika maeneo ya Gongo la Mboto (Mtaa wa Banana), Manzese, Mbagala (Zakhem), Tabata Kinyerezi, Mbezi Mwisho Luis, Mbezi Tanki Bovu, Mwenge, Masaki, Kariakoo (Mtaa wa Uhuru na Nyamwezi), na Jamhuri Posta .
Vituo hivi vimewekewa timu mahiri ya huduma kwa wateja na miundombinu inayowezesha utoaji wa huduma bora kwa wakati wote. Vituo vinafunguliwa kuanzia saa 2 Asubuhi mpaka saa 2 usiku, siku za Jumatatu mpaka Jumamosi, na saa 2 Asubuhi mpaka 11 jioni siku ya Jumapili.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!