
MAGAZETI ya Leo Ijumaa 09 May 2025
MAGAZETI ya Leo Ijumaa 09 May 2025
Klabu ya Simba imetajwa kuwa katika mchakato wa kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa Azam Fc, Feisal Salum ‘Fei Toto’
Inaelezwa kuwa juzi Rais wa heshima wa Simba Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ alifanya mazungumzo na Wawakilishi wa Fei Toto ambapo kimsingi ‘tajiri’ amempa Fei ofa nono ya mshahara na dau la usajili
Hatua iliyobaki ni kukamilisha mazungumzo na Azam Fc ambayo bado inamkataba wa mwaka mmoja na Feisal ambaye alijiunga nayo misimu miwili iliyopita akitokea Yanga SC.
Simba ina uhakika wa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao wa 2025/2025 na malengo yao ni kufanya vyema kama walivyofanya msimu huu katika michuano ya kombe la Shirikisho ikitinga Fainali ambapo itacheza na RS Berkane.
Feisal amekuwa ‘injini’ ya Azam Fc katika misimu miwili akifunga mabao 23 na kutoa pasi 21 za mabao.
Aidha Jean Charles Ahoua ndiye tegemeo katika la kiungo cha ushambuliaji cha Simba lakini ni wazi imeonekana eneo hilo linahitaji kuongezewa nguvu, huku Feisal akiwa ndiye kiungo bora wa ushambuliaji kwa sasa katika Ligi Kuu ya Tanzania.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!